ZITTO KABWE, DKT. KITILA MKUMBO WAFUNGUKA KUHUSU KUVULIWA MADARAKA CHADEMA ''SING'OKI NG'OOO CHADEMA''-ZITTO
'Waliokuwa
Naibu Katibu Katibu Mkuu na Makamu Mwenyekiti' wa Chadema, Zitto Kabwe
(kulia) akizungumza kwa hisia wakati alipokuwa akitoa tamko rasmi
kuhusu 'maamuzi magumu', yaliyochukuliwa na chama chake kwa kuvuliwa
madaraka ya ndani ya chama hicho kwa kile kilichoelezwa kuihujumu
Chadema.
**********************************
*Zitto Asema Hatoki Chadema, Dk. Kitila Akiri Kuandaa Waraka wa Siri.
Na Joachim Mushi, Dar
MBUNGE
wa Chadema na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Zitto
Kabwe amesema hawezi kufanya maamuzi magumu ya kutoka ndani ya chama
hicho kwa kile kilichotokea ndani ya chama hicho. Amesema yeye atakuwa
wa mwisho kutoka Chadema na si vinginevyo.
Zitto
ameyatoa hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam alipokuwa anazungumzia maamuzi ya Kamati Kuu ya Chadema ya kumvua
nafasi zake zote za uongozi yeye pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya
chama hicho Dk. Kitilla Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa
Arusha Samson Mwigamba.
Zitto
Kabwe na Kitila Mkumbo wakiingia Ukumbini katika Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam, mchana huu kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa
habari.
***************************************
Zitto
amekana kuhusika wala kuujua waraka wa siri ambao ndiyo uliosababisha
kumvua madaraka baada ya uamuzi wa Kamati Kuu ya chama kuunasa waraka
huo.
"Mimi
nimeusikia ule waraka kwa mara ya kwanza kwenye Kamati Kuu na
nilisikitika sana kwa nini haukunifikia haraka kwani ningeanza
kutekeleza mara moja." alisema Zitto akizungumza.
Huenda
leo watu walitegemea nitafanya maamuzi magumu ya kuondoka kwenye chama;
"Mimi bado ni mwanachama wa Chadema na nitakuwa wa mwisho kutoka kwenye
chama hiki kwa hiyari yangu, nitafanya taratibu zote za chama
kuhitimisha jambo hili mimi sitoki kwenye chama hiki labda wanitoe wao,"
alisema Zitto.
Zitto
alisema anaumia sana anapotuhumiwa kwa kuwa yeye ni binadamu.
"...ninapotuhumiwa naumia ninapoambiwa naujumu chama hiki naumia kwa
kuwa nakipenda chama na nimekitumikia muda mrefu. Aidha aliwataka
viongozi wa Chadema kuacha siasa za uzushi ili kujenga chama himara na
kuwakomboa Watanzania.
"...Sisemi
kama mimi sina makosa ni binadamu nimefanya mambo mengi kwa chama
changu, lakini kinachoendelea kwa sasa ndani ya chama chetu ni mapambano
ya kukuza demokrasia na ni mapambano ya wanaotaka mabadiliko na
wasiopenda mabadiliko ndani ya chama...mapambano ya wawajibikaji na
wasiopenda kuwajibika ni mapambano ya wanaopenda demokrasia na
wanaokwaza demokrasia." alisema Zitto huku akionesha kusikitishwa.
Zitto
Kabwe (kulia) na Dk. Kitilla Mkumbo, wakisikiliza kwa makini maswali
yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo.
Umakini katika kusikiliza maswali.......
Zitto Kabwe, akiagana na baadhi ya waandishi wa habari wakati akiondoka ukumbini.
No comments:
Post a Comment