KINANA HADI KYELA KWA MELI
Baadhi
ya abiria waliosafiri na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana katika
Meli ya Mv Songea, alipokuwa akitokea Mbamba Bay mkoani Ruvuma kwenda
Kyela mkoani Mbeya. Meli hiyo iliyoanza kazi katika Ziwa Nyasa, mwaka
1974, ina uwezo wa kubeba abiria 213 wakiwemo wafanyakazi 13 wa meli
hiyo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.
Nahodha
wa mv Songea Tom Faya akimpatia maelekezo ya namna meli hiyo
inavyofanya kazi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake,
wakati katibu mkuu huyo alipokuwa akisafiri na meli hiyo kutoka Mbamba
Bay mkoani Ruvuma kwenda Kyela mkoani Mbeya, leo Nov 24, 2013. Kulia ni
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na
Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. Kwenye usukukani ni Nahodha
Msaidizi, Conrad Shauritanga.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Mbeya Godfrey Zambi, baada ya kushuka katika Mv Songea, baada ya
kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya
akitokea Mbamba Bay, Songea, leo.
Waziri
wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe
akimlaki wa furaha, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipompokea
katibu mkuu huyo, baada ya kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira,
wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24,
2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu
wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi, baada ya
kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya
akitokea Mbamba Bay, Songea, leo.
No comments:
Post a Comment