|
Said A. Arfi (MB) |
Salaam,
Napenda
kuwasilisha kwako (Mwenyekiti Taifa CHADEMA) taarifa ya kujiuzulu
nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa
kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia
kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na
Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari
kuchaguliwa marafiki.
Kwa
kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka
mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu. Pamoja na kulijadili katika
vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita
bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo
lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa
mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki wa kupindukia.
Aidha
mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei
kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu
na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi
wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali
binafsi.
Kwa
kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu
katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu
Nawasilisha.
Said A. Arfi (MB)
No comments:
Post a Comment