MIIIIIIIIIIIIII

Thursday, October 24, 2013

d
AJALI hii imetokea mchana huu maeneo ya Mbagala Chamanzi Magengeni na kusababisha Dereva wa Pikipiki almaarufu kama Bodaboda kupoteza viungo.. Vyanzo vya ajali hio vimeieleza website hii kwamba ajali hio ilasababishwa na mwendo mkali wa pikipiki yenye namba za usajili T752 CHW uliopelekea pikipiki hio kuingia Chini ya Lori hilo lenye namba za
usajili T152 BKX, Japo dereva wa pikipiki alijitahidi kufunga breki lakini jitihada zake hazikufanikiwa alijikuta uvunguni mwa Lori,





ALIOVAA singlend nyeupe hapo pichani ni Dereva wa lori akisimulia chanzo cha ajali.. Alisema kwamba yeye alivyokata kona ghafla alimuona jamaa wa pikipiki kwa mbele yake akiwa katika mwendo kasi sana ndipo alipojaribu kumkwepa kwa bahati mbaya maji yalizidi unga kila mmoja alitaka kumkwepa mwenzake mara wakakutana uso kwa uso hatimaye Dereva wa pikipiki kuvunjika mikono papohapo, Mpaka muda huu yupo hospitali Endelea kutembelea website hii ya www.masainyotambofu.com kupata taarifa za majeruhi.


 DU...! balaa...!!!
 WANAFUNZI nao walikwepo eneo la tukio.
RAIA wakishangaa shangaa katika eneo la tukio...!!!



 HUWEZI amini kama dereva wa Pikipiki kanusurika...!

 HAPO ndio wamelitoa Gari Pikipiki nyang'anyang'a..!
 KAMA kawaida mapaparazi wa kujitegemea walikwepo...! Yani sehemu yeyote ya tukio watu kama hawa hawakosekanagi.

PICHANI ni Trafic poloce akipima ajali hio baada ya dereva wa Bodaboda kuwahishwa Hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi. 

MADEREVA wa pikipiki aina ya Bodaboda muwe makini barabarani kuepuka ajali zisizo na lazima. Ujumbe huu umeletwa kwenu kwa hisani ya www.masainyotambofu.com
PICHA hizi ni kwa hisani ya (mussa habibu) mdau wa website hii ya MASAI NYOTAMBOFU
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment