SERIKALI IPUNGUZE MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA-KINANA
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya
Masoko ,kijiji cha Lupando wilaya ya Rungwe ,Katibu Mkuu waliwaambia
wananchi hao kuwa urasimu na umangi meza wa watendaji wa serikali ndio
unachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha maendeleo yao nyuma na kusema
kamwe CCM haitokubali hali hiyo iendelee na kusisitiza CCM itahakikisha
wananchi wanapata haki zao za msingi kwanza.
Mwakilishi
wa Wananchi wa Kijiji cha Lupando Ndugu Wema Mwaipopo akiomba sana kwa
niaba ya wananchi wake watatuliwe suala la maji,umeme na barabara kwani
hizo ndio zilikuwa ahadi kubwa za Mbunge na Rais.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya
Masoko kijiji cha Lupando na kuwaambia wananchi kuwa wapinzani ni sawa
na Jogoo hata aamke saa ngapi hawezi fungua mlango,na kuwasisitiza
wananchi wa kijiji hicho ni CCM pekee inayoweza kuwazungumzia na kero
zao zikatatuliwa. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Asumwisi
Asagwile Mwatebela ,Mlezi wa Vijana wa Chadema wilaya ya Rungwe
akirudisha kadi yake kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na
kujiunga rasmi na CCM.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kiwira Rungwe
na wakati wa ufunguzi wa vikundi viwili vya wajasiriamali ambapo
aliwaambia vijana maendeleo yanaletwa kwa kufanya kazi kwa kujituma na
waondoe mawazo kuwa Katiba mpya ndio itakuwa mwarobaini wa matatizo yao.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia maabara ya shule ya
Sekondari ya Ikuti ikiwa moja ya sehemu ya ahadi ya serikali ya kujenga
maabara katika kila shule ya Sekondari ya Kata.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Nyumba za walimu wa shule ya Sekondari Ikuti wilayani Rungwe.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmani Kinana akiongozana na Mkuu wa Shule ya
Ikuti Ndugu Emmanuel Ngasa pamoja na viongozi wengine wa chama na
serikali baada ya kukagua jengo la hosteli la shule ya sekondari ya
Ikuti.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa shina
namba 2,Butonga Tawi la Ikuti kwa Balozi James Mbasi, na kusisitiza
viongozi wote wa CCM waige mfano wa Mabalozi kwani wanafanya kazi kwa
kujitolea katika kukiimarisha na kukijenga chama.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahama Kinana akikata utepe kama ishara ya
kuwasha umeme katika kituo cha Afya cha Ikuti wilayani Rungwe.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na viongozi wa wilaya
ya Rungwe pamoja na wananchi kuelekea kwenye uwanja wa mkutano Ikuti.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Wilaya Ndugu Richard Kasesela akipiga ngoma ya
Kitongo kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ikuti
ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mbunge
wa Viti Maalum Wananwake mkoa wa Mbeya Dk.maru Mwanjelwa akicheza
ngoma kabala ya kuanza kwa mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Ikuti
ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wa
kitaifa aliofutana nao Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
Dk.Asha-Rose Migiro na Katiibu wa NEC Itikadi na Uenezi walihutubia.
Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Dk.Mary Mwanjelwa akihutubia wakazi wa
kata ya Ikuti na kuwaambia wanawake waandae vikundi vyao kwani Benki ya
wanawake karibia itafunguliwa hivyo fursa za kupata mikopo zitaongezeka
na kusaidia kufanya biashara kwa ufanisi na kuleta maendeleo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Ikuti
wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya na kusema serikali ipunguze matumizi
yasiyo na lazima na badala yake nguvu nyingi iletwe kwa wananchi katika
kuwaletea maendeleo.
Wakazi
wa Ikuti wakiwa juu ya mti wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi
wao ambazo nyingi zilijibiwa vizuri hasa suala la umeme ambalo wananchi
wanaweza kulipa kidogo kidogo.
Dk.Mary
mwanjelwa akizungumza na akina Mama wauza ndizi wa kijiji cha Iponjola
kata ya Rufingo wilaya ya Rungwe na kuwataka waanzishe vikundi kwani
benki ya wanawake ipo karibuni kufunguliwa katika mkoa wa Mbeya hivyo
itawasaidia kupata mikopo kwa riba nafuu.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alisimama kuwasalimu wakina mama
hao kisha kuutambulisha uongozi wote aliokuwa nao kwenye msafara.
No comments:
Post a Comment