YALE YALEEEEE!!!!! MWENYEKITI WA SIMBA ADEN RAGE, JULIO NA KIBADEN, WAPIGWA STOP SIMBA, ZADRAVOK NA MATOLA KUONGOZA JAHAZI
BAADA ya wanachama wa Simba kuhaha kutaka kumng’oa
madarakani Mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage sasa dua zao zimetimia baada ya
Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kumsimamisha rasmi.
Kikao hicho kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam
kilifikia maamuzi hayo kutokana na madai ya kuwa kiongozi huyo wa juu wa Simba kukiuka
miiko ya uongozi na kukiuka katiba ya klabu hiyo.
Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Rage
kuwasainisha mkataba wachezaji wawili kutoka Zanzibar Ally Badru na Awadh Juma
aliyekuwa anacheza Mtibwa.
Mabosi wa Simba wamethibitisha kusimamishwa kwa Rage
na muda huu wanazungumza na waandishi wa habari sababu za kuchukua maamuzi hayo
magumu.
Taarifa ya awali inadai kuwa Rage amekuwa
hajishughulishi kwa karibu na timu hiyo lakini pia amekuwa akikiuka baadhi ya
mambo ndani ya katiba na ndio maana kamati ya utendaji imepata nguvu ya
kumsimamisha kwenye kikao hicho cha jana.
Wakati
mwenyekiti huyo na makocha wa timu hiyo, wakitimuliwa, sasa jahazi la
Simba linatarajia kuwa chini ya Kocha mpya kutoka Croatia, aliyekuwa
akiinoa timu ya Gol Mahiya ya Kenya, Zadravok Logarusic, ambaye atakuwa
akisaidiwa na kocha msaidizi, Suleiman Matola.
No comments:
Post a Comment