CAMEROON HAOOOOOOO, KOMBE LA DUNIA 2014 WAIBANJUA TUNISIA MABAO 4-1
Nahodha
wa timu ya Cameroon,Samuel E'too, akishangilia baada ya timu yake
kujikatia tiketi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia 2014, kwa
kuibanjua Tunisia mabao 4-1.
TIMU
ya Cameroon jana imeungana na Ivory Coast na Nigeria kwa timu za Afrika
kufuzu kutinga fainali za kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil baada
ya kuwaadhibu Tunisia kwa jumla ya mabao 4-1 mjini Yaounde, ambapo sasa
ni mara ya saba mfululizo kwa timu hiyo kutinga fainali hizo.
Mwezi
uliopita wakati mataifa hayo mawili yalipokutana katika uwanja wa Rades
, nchini Tunisia matokeo yalikuwa suluhu ya kutofungana.
Lakini
katika mechi iliyochezwa mjini Yaounde, jana Jumapili, mshambuliaji
Pierre Webo, ndiye alikuwa wa kwanza kufungua ubao wa mabao baada ya
kuchambua vilivyo na kuipenya safu ya ulinzi ya Tunisia.
Bao
la pili liliweka kimiani na Benjamin Moukandjo, kabla ya timu hizo
kwenda mapumziko, huku mchezaji wa akiba Ahmed Akaichi, akiipatia
Tunisia bao la kufutia machazi na la pekee muda mfupi baadae.
Lakini
kabla ya kipyenga cha mwisho, mchezaji Jean Makoun, aliiongezea
Cameroon mabao mawili ya chap chap na kufanya matokeo kuwa 4-1 hivyo
kuipa Cameroon tiketi ya kuwa timu mojawapo zitakazo wakilisha Afrika
katika kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014.
Awali
,timu za Ivory Coast na Nigeria zilikuwa tayari zimejikatia tiketi ya
kuwa wawakilishi wengine wa Afrika katika mashindano hayo ya mwaka 2014.
Mashabiki
wa Soka wa Cameroon, wakishangilia timu yao baada ya kujikatia tiketi
ya kufuzu Kombe la Dunia 2014, katika mchezo wao wa jana ilipoibanjua
Tunisia, jumla ya mabao 4-1
No comments:
Post a Comment