WATU WANNE WAFARIKI DUNIA NA 28 MAJERUHI KATIKA AJALI YA LORI MKOANI TABORA. mfaumehamisi@gmail.com
Ajali hiyo inahusisha gari lenye namba za usajiri T 829 AHH iliyokuwa ikielekea katika soko la wiki maarufu kama MNADA. Gari hilo aina ya lori limepata ajali maeneo ya kijiji cha Ilolanguru mbele kidogo ya chuo cha kilimo cha Tumbi kuelekea Urambo kwenye muda wa saa 4 asubuhi.
Dk. Kitapondya Deus, Mganga mfawidhi hospitali ya Rufaa ya Kitete mkoani Tabora, ameuambia mtandao huu kuwa wamepokea wahanga 28 wa ajali hiyo na miili minne (4) ya marehemu ambao tayari wametambulika na ndugu zao. Pia mganga amesema wagonjwa wengine watasafirishwa na kupelekwa hospitali ya karibu ambayo ni Nkinga.
Miili minne ya waliofariki katika ajali ya lori la mnada ambayo tayari imetambuliwa na ndugu zao.
Miili minne ya marehemu waliokumbwa na ajali ya lori la mnada
Wananchi waliojitokeza kushuhudia wahanga wa ajali ikiwa pamoja nakuwatambua ndugu zao waliohusika katika ajali hiyo.
Dereva anayehusika na ajali hiyo amekwishatiwa mbaroni na jeshi la polisi. Chanzo cha ajali hiyo inasemekana kuwa na ubovu wa gari hilo ambalo lilikuwa na tairi lilokwisha (kipara)
PICHA ZA ENEO LA TUKIO ZITAWAJIA KWA HISANI YA MTANDAO WA KapipiJ Habari
No comments:
Post a Comment