Ibra wa “Wakali Danta” auawa kwa kuchomwa kisu ktk kugombania demu aitwaye Fatma Kiduku
. Tukio hilo la kusikitisha limetokea Julai 27, mwaka huu maeneo ya Magomeni Kagera ambapo ndugu wa Ibra, Ally Jumanne Sanane alidai kuwa, Ibra alichomwa kisu na kijana aliyefahamika kwa jina la Kelvin wakimgombea demu aitwaye Fatma Kiduku.
Mtoa habari huyo alidai: “Fatuma alikuwa ni mchumba wa Ibra lakini pia inaonekana alikuwa akitoka na Kelvin.
“Ibra alipofika ndiyo akaanza kupigana na Kelvin, kuona amezidiwa Kelvin alitoa kisu na kumchoma cha kwanza kisha cha pili na ndiyo Ibra akaanguka chini na hakuamka tena,” alidai mtoa habari huyo.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo lilitokea Julai 27, saa 9:30 eneo la Brazil Magomeni Kagera.
Mbali na Kelvin pia mwanamke ambaye ndiye chanzo cha tukio hilo naye anasakwa.
Kesi hiyo imefunguliwa jalada namba MAG/IR/5600/ 2013 MAUAJI.
Uchunguzi wa jeshi la polisi unaendelea zaidi ili kuweza kuwakamata wahusika waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
SOURCE-GPL




No comments:
Post a Comment