AJALI YA AJABU DAR LEO, GARI LANING'INIA JUU YA MTI
Gari
lenye namba za usajiri T 857 BAR, likiwa limening’inia juu ya mti
katika daraja la Kawe lililopo Mbezi kwa Komba Dar es Salaam jana.
Haikuweza kufahamika chanzo cha ajali ya gari hilo, kwa mujibu wa
walioshuhudia ajali hiyo walieleza kuwa ajali hiyo ilitokea usiku wa
kumakia leo mida ya saa tisa usiku katika daraja hilo.
Huu
ni upande wa chini ya gari hilo linavyoonekana likiwa juu ya mti,
ambapo imeelezwa magari kadhaa yalifika kutoa huduma ya kuliondoa mahala
hapo bila mafanikio.
Askari
wa usalama barabarani, akiongoza magari ili kuondoa foleni ambayo
ilikuwa ikisababishwa na madereva waliokuwa wakishangaa ajali hiyo jambo
ambalo lilimfanya kila dereva kupunguza mwendo afikapo eneo hilo.
No comments:
Post a Comment