MIIIIIIIIIIIIII

Monday, April 7, 2014

Hivi ndivyo Diamond alivyowa-sapraiz Mashabiki wake kwenye uzinduzi wa video ya Queen Darlin.

Ukubwa wa jina la Diamond ndiyo hufanya mahali popote Tanzania anapotokea au kuonekana kuwa na hali isiyo ya kawaida,Usiku wa kuamkia April 07 Club Bilicanas kulikua na uzinduzi wa video ya Queen Darlin ambaye ni dada wa Diamond Platnumz.

Wakati burudani zikiendelea mashabiki wakiwa hawajui kilichopo backstage ndipo Diamond alipopanda kulitokea shangwe kubwa na kuna shabiki mwingine alikuja kwa kasi kutaka kumkumbatia inawezekana ni furaha iliyozidi kipimo kubwa zaidi ni shabiki ambaye alitoa machozi kisa kikiwa ni kutaka kupiga tu picha na Diamond.

Hizi ni baadhi ya picha ya show hiyo zikimuonyesha na mastar kadhaa waliokuepo akiwemo Shettah.














Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale.

mfaume hamisi

SHOWROOM YA MAGARI YAUNGUA JIJINI DAR


Duka la Magari (showroom) iliyokuwa karibu na eneo la Mlimani City barabara ya Samnujoma jijini Dar es Salaam imeteketea kwa moto na kusababisha hasara ambayo bado haijafahamika, ambapo mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijafahamika.Magari yakiwa yameteketea kwa moto.

Hapa moto ulikuwa ndiyo umeanza kuwaka kabla ya kuanza kuunguza magari.
Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale.

Saturday, February 22, 2014


Saturday, February 22, 2014

SPORT'S NEW'S: YANGA 7 RUVU SHOOTING 0 KIPIGO KITAKATIFU


Dakika ya 80, Saimon Msuva anaipatia Young Africans bao saba

Dakika ya 75, Ruvu Shooting 0 - 6 Young Africans

Dakika ya 70, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la sitaDakika ya 69, anaingia Juma Abdul kuchukua nafasi ya Mbuyu Twite

Dakika ya 54, Didier Kavumbagu anaipatia Young Africans bao la tanoDakika ya 30,Ruvu Shooting 0 - 4 Young Africans

Dakika ya 30, Mrisho Ngasa anaipatia Young Africans bao la nne

Dakika ya 27, Emmanuel Okwi anaipatia Young Africans bao la tatu

Dakika ya 2, Saimon Msuva anaipatia Young Africans bao la pili

Sekunde ya 40, Didier Kavumbagu anaipatia Young Africans bao la kwanza.

YANGA LINE
-UP: Deogratias Munish -30, Mbuyu Twite - 6, Oscar Koshua - 4, Nadir Haroub - 23, Kelvin Yondani - 5, Frank Domayo - 18, Saimon Msuva - 27, Mrisho Ngasa - 17, Didier Kavumbagu - 7, Emmanuel Okwi - 25, Hamis Kizza - 20

Subs:Juma Kaseja - 1, Juma Abdul - 12, David Luhende - 3, Rajab Zahir - 14, Athuman Idd - 24, Hassan Dilunga - 26, Said Bahanuzi - 11

RUVU SHOOTING LINE
-UP: Abdallah Ramadhani, Michael Aidan-20, Stephano Mwasyika-21, Mangasini Mbonosi-21, Shabani Suzan - 24, Alli Kani Mganda- 14, Hamis Ismail-17, Juma Nade-5, Elias Maguli-10, Lambele Jerome-11, Cosmas Lewis-3

Sub:Mahamudu Mbulu-18, Mau Boffu-3, Gidion Sepo-22, Ayoub kitala-7, Juma Mdini-13, Said Dilunga-15

Thursday, February 13, 2014

kutoka .sufiani mafoto

*WATATU WAHOJIWA NA KAMATI YA MAADILI YA CCM MJINI DODOMA

 Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa akizungumza na Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye kabla ya kuanza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma.

Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye akiwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma tayari kwa kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili.
 Ndugu William Ngeleja akisubiri kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama.
 Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa kizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi ambapo alisema mazungumzo yalikuwa mazuri,yalikuwa yenye nia ya kukijenga chama kwa ajili ya uchaguzi 2015.
Waandishi wa Habari wakiwajibika kuandika habari nje ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi ambapo viongozi watatu walihojiwa na Kamati ndogo ya Maadili.
***************************
Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Phillip Mangula  leo imewahoji watu watatu ambao wawili walishawahi kuwa Mawaziri Wakuu katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. 

Mawaziri hao waliohojiwa leno ni Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa,Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye na Mbunge wa Sengerema Ndugu William Ngeleja ambaye pia alishawahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

 Kamati hiyo bado ina kazi ya kuwahoji viongozi wengine watatu ambao leo walishindwa kufika baada ya kuomba hudhuru kwani walikuwa na majukumu mengine ya kiserikali, ambao hawajafika leo ni Waziri wa Mambo ya Nje Ndugu Bernard Membe ambaye yupo safarini nje ya nchi ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Ndugu Stephen Wassirana Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Ndugu Januari Makamba.